Bandari kuwaalika Mathare Mombasa

Taifa Jumapili

TIMU ya Bandari FC hivi leo Jumapili inakabililana na Mathare United FC kwenye pambano linalotarajiwa kuwa kali la Ligi Kuu ya Kenya (KPL) litakalochezwa uwanja wa Kaunti ya Mombasa. Bandari ilishindwa kutamba III- popambana na Nakuru All Stars na kutoka sare ya kufungana bao 1-1, inatarajia kucheza kufa kupona kuwafurahlsha mashablki wao ambao hawajaridhika na jinsi tlmu inavyocheza Japo Ina wanasoka kadhaa wa timu ya taifa ya Harambee Stars. Lakini msemajl wa Bandarl FC, Ernest Mbalanya alifahamisha Taifa Leo jana kuwa vijana wake watarekebisha makosa madogo madogo na kuhakikisha wameshinda mechi hiyo wapate kupanda kwenye jedwali la ligl kuu. Mashabiki watatakiwa 11 kulipa Sh. 100 za kiingllio kwa sehmu zote. “Nawaomba mashabiki wengi wajitokeze kuwashangilia wachezajl ili timu yetu ipate ushindi dhidi ya Mathare,” alitoa ombi Mbalanya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bandari Fan Club (BFC). Mbalanya pia alitangaza kuwa kutakuwako na kuflandikisha kwa wanachama wa BFC bila ya malipo yoyote. “Tulikuwa tufanye hivyo wakati wa mechi ya All Stars lakini kubadilika kwa wakati wa kuanza kwa mechi hiyo kulitufanya tusiandikishe,” alisema afisa huyo wa Bandari.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*