Bandari wajikita jijini kuinolea Mathare Utd

Baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Thlka United, Bandari FC imeamua kubakia jijini Nairobi kusubiri mechi yake nyingine ya Ligi Kuu ya Kenya (KPL) dhidi ya Mathare United itakayofanyika uwanja wa Nyayo Ijumaa. Msemaji wa klabu hiyo, Ernest Mbalanya aliambia Taifa Leo kwa njia ya simu jana kuwa klkosi cha Bandari cha wanasoka 18 kimebakia Nairobi baada ya mechi dhidi ya Thika kwa sababu kimepangiwa kukutana na Mathare hapo Ijumaa. “Kutokana na kubakia siku chache za mechi dhidi ya Mathare, tumeonelea vizuri wanasoka wetu wafanye mazoezi jijini Nairobi kwa sababu kurudi nyumbani ni safari ndefu ya kuchosha,” akasema Mbalanya. Alisema wachezaji hao wamebakia Nairobl na wanafanya mazoezi chini ya mkufunzi wao, Twahir Muhiddin kwa ajili ya kujitayarisha kwa mchezo wao wa Ijumaa na Mathare.Taifa Leo

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*