Kingilio bure:Mechi ya Bandari FC na KCB FC, Mbaraki

Kingilio bure Bandari wasoka wa Mkoa wa Pwani wanatarajia kushuhudia mechi ya timu yao ya Bandari FC na wageni wao KCB bila malipo pale timu hizo zitakapokutana katika mechi ya Ligi Kuu ya Kenya (KPL) hivi leo latika uwanja wa Kaunti ya Mombasa. Bandari inatarajia kushinda pambano hilo ikiwa mchezo iliocheza dhidi ya Sofapaka na kutoka sare ya kufungana mabao 2-2 utakuwa kama kigezo. Msemaji wa Bandari FC, Ernest Mbal- anya aliwapongeza wachezaji wa timu yake kwa kucheza vizuri mechi zao mbili za ugenini ingawa walipoteza mchezo wa kwanza kwa kushindwa 2-1 na Gor Mahia. “Nina matumaini makubwa kwa timu yetu kuitambia KCB. Tumeondoa malipo tukitarajia mashabiki wetu wengi watajitokeza na kuwashangilia vijana wetu wapate ushindi,” akasema Mbalanya ambaye pia ni mwenyekiti wa kundi la mashabiki la Bandari Fan Club. Msemaji huyo wa Bandari anasema hana shaka wachezaji wao watawapa mashabiki wao burudani na ushindi. “Tumerudi na pointi moja kutoka ugenini na tuna matarajio makubwa ya kunyakua pointi zote tatu Jumatano,” akasema. Mbalanya anasema kuondoa ki ingilio kutavutia mashabiki wengi ambao wanaopenda uwanja huo ulio karibu nao. “Nina hakika wapenda soka wa Mom- basa na Pwani kwa ujumla watajitokeza kuwashangilia wachezaji wetu ambao wamepigana kiume dhidi ya timu kubwa.”

Source: Taifa Leo by ABDULRAHMAN SHERIFF

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*