Mashabiki waisifu SportPesa

Mashabiki waisifu kampuni kuwapa basi kusafiri Nairobi BANDARI Fan Club (BFC), jana ilishukuru SportPesa kwa kutoa basi moja itakayowachukua mashabiki wa soka watakaosafiri hadi Nairobi kuishangilia timu yao inapokutana na St Eloi Lupopo ya DR Congo kwenye mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho la Bara Afrika hapo Jumapili. Mwenyekiti wa BFC, Ernest Mbalanya alisema anaishukuru sana SportPesa kwa kujitolea basi moja itakayowasafirisha mashabiki 45 huko Nairobi kuishangilia timu yao ya Bandari FC dhidi ya Lupopo kwenye mechi ambayo timu hiyo ya Pwani itahitaji kushinda kwa zaidi ya mabao mawili.
Mfano mzuri wa kuigwa “Tunaishukuru SportPesa kwa kulipia basi moja na ni mfano mzuri unaohitajika kuigwa na mashirika, makampuni ya kibinafsi na wafanya biashara ili mashabiki wengi waweko uwanja wa Nyayo siku ya Jumapili wachezaji wetu wacheze kwa ari ya ushindi,” akasema Mbalanya. Mbalanya ambaye pia ni Msemaji wa Bandari FC alisema mashabiki hao wataondoka ke- sho Jumamosi usiku na kurudi siku ya Jumapili usiku baada ya kuchezwa kwa mechi hiyo.
Wakati huo huo, timu ya Bandari FC ya wachezaji 20 iliondoka jana asubuhi kuelekea Nairobi ambapo itapiga kambi kwa zaidi ya siku saba kwa ajili ya mechi mbili, moja ya barani Afrika dhidi ya Lupopo na nyingine ya Ligi Kuu ya SportPesa na AFC Leopards Jumatano ijayo. “Nina imani kubwa vijana wangu watatekeleza wajibu wao kwa kuishinda Lupopo kwa idadi ya mabao yatakayotusaidia ku- songa mbele mashindano ya Af- rika na pi kuhakikisha tunapata pointi zote tatu za ligi kuu dhidi ya Leopards,” akasema Kocha Mkuu Twahir Muhiddin. Muhiddin anasema uzuri wa ziara hiyo ya jijini Nairobi ni kwamba wachezaji wote wako katika hali njema ya uchezaji na afya zao na ana uhakikia watacheza kwa ari na moyo wa kupata ushindi katika mechi zote mbili.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*