Wachezaji wote 30 kusafiri kwa mechi dhidi ya Ulinzi Stars.

Wachezaji wa Bandari wadhaminiwa baada ya matokeo bora Ligi Kuu kutokana na kufanya vyema kwenye Ligi Kuu ya msimu huu, wadhamini wa klabu ya Bandari FC, Shirika la Bandari za Kenya (KPA) limewatunukia wachezaji wote 30 wa kikosi cha timu hiyo wasafiri kwenda Nakuru kwa mechi yao ya mwisho dhidi ya Ulinzi Stars FC.

Msemaji wa klabu hiyo ya Bandari, Ernest Mbalanya alisema kuwa kutokana na kuwa katika nafasi ya tatu kwenye ngazi ya Ligi Kuu, KPA imeamua kuwapa fursa wachezaji wote 30 kwenda Nakuru badala ya kikosi cha wachezaji 18 pekee. Wakati huo huo, Mbalanya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bandari Fan Club anasema mashabiki kadhaa wanatarajia kusafiri kuelekea Nakuru kuishuhudia timu hiyo ikicheza na Ulinzi Stars hapo Jumapili na pia Alhamisi ijayo kwenye mchezo wa GOtv Shield. Mbalanya ana matumaini makubwa ya timu hiyo kufanya vyema kwenye mechi hizo mbili na hata kupata ushindi. Wachezaji wetu wana mor- ali na hakuna ajabu kama tutashinda Jumapili,”Taifa Leo

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*