🔥 Siraj "Mastermind" Mohamed, mchezaji mwenye sifa ya kukukusanya kijiji kizima, pamoja na mwenyekiti na mbunge, ndiye anayetupambia simu zetu wiki hii.
Kuna wakati alimfanyia maajabu beki wa timu fulani (jina tumelibana) akashikwa na kisunzi, akakaa chini kama mkunaji nazi, baadaye kidogo alisikika akimwambia, "Malipo ni hapa hapa duniani."
Tunapoingia katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, Tunawatakia nyote, Mwezi uliojaa baraka, Allah, ajibu dua zetu sote, atujalie Kheri na atuzidishie neema.